Hebrews 9:26-28

26 aIngekuwa hivyo, ingempasa Al-Masihi kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. 27 bKama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu, 28 cvivyo hivyo Al-Masihi alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.
Copyright information for SwhKC